Ijumaa, 17 Juni 2016

SERIKALI YAONGEZA MUDA KWENYE MADUKA MAKUBWA DAR ES SALAAM

DAR ES SALAAM
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam inakusudia kuruhusu baadhi ya maduka makubwa kutoa huduma zaidi ya muda wa kawaida wa maduka kufungwa ili kutoa fursa kwa wafanyakazi kupata huduma hiyo pindi wanapotoka makazini.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda  alipomwakilisha Makamu wa Rais kwenye hafla ya Futali iliyoandaliwa na Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam.
Makonda alisema kuwa kusudio hilo linatokana na changamoto ya upatikanaji wa nafasi ya kupata huduma hiyo kwa wafanyakazi  kwani uchelewa kutoka maofisini jambo lilalosababisha baadhi ya wafanyabiashara kupeleka bidhaa zao huko huko ofisini.
Aliongeza kuwa amekusudia kufanya mambo muhimu matatu katika kipindi hiki cha mwenzi mtukufu wa ramadhani ambapo aliyataja mambo hayo kuwa ni kuongeza muda wa kufunga maduka hasa yale makubwa (malls), kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma na kupambana na watumiaji wa usafiri wa pikipiki wanaokiuka sheria ya matumizi ya Kofia ngumu (helmet).
“Nimekusudia kufanya mambo muhimu matatu ndani ya mwezi huu mtukufu wa ramadhan, niwadokeze tu kuwa mambo hayo ni pamoja na kuongeza muda wa kufanya biashara kwa maduka makubwa (shopping malls), kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma na kupambana na wavunjifu wa sheria ya matumizi ya helmet.” Alisema Makonda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania Bibi. Ineke Bussemaker alisema kuwa wao kama Taasisi ya Kifedha imekuwa na desturi ya kuwajali wateja wao hivyo wanatumia fursa hii kushiriki pamoja na wateja wao walio katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kuwatia moyo wakustahilifunga hiyo muhimu katika uislamu.
Aidha aliongeza kuwa NMB itaendelea kushirikiana na jamii mbalimbali katika kuhakikisha inasaidia pale panapohitajika msaada wao kama ambavyo wamekuwa wakitoa misaada katika kuchangia huduma za kijamii kama vile madawati.

p.txt

MJASILIAMALI MERCY KITOMARY ANATAMANI KUKUTANA NA RAISI MAGUFULI

DAR ES SALAAM

MJASIRIAMALI kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari amesema anatamani kukutana na Rais John Pombe Magufuli kumwelezea haja ya kukutana na wanawake wajasiriamali vijana wamweleze matatizo yao.
Amesema Rais baada ya kukutana na makundi mbalimbali ya wafanyabiashara , inafaa akutane na wajasiriamali wanawake vijana ambao wanapita katika magumu mbalimbali .
Alisema katika mahojiano hivi karibuni ambayo sehemu yake itachapishwa katika mtandao wa Modewjiblog muda wowote kwamba, rais Magufuli akiwa kama ‘Role Model wake’ katika kujituma, anaweza kuwasikiliza wanawake hao vijana na kusaidia kuwasukuma juu zaidi katika kampeni ya kuiweka Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
“Nimekuwa nikikutana na wanawake wenzangu ambao wamekata tamaa na wamekuwa wakiniuliza ninawezaje kuendelea, nikawambia wasi-give up (wasikate tama) na kwamba serikali hii ni ya viwanda na kuchapa kazi “ alisema na kufafanua kwamba wanachohitaji wanawake hao ni mazingira mazuri ya kufanya ujasiriamali.
Mercy ambaye anatengeneza ‘ice cream’ zinazotumia matunda yote ya kitanzania kama vile fenesi, nanasi, bungo, ndizi, embe ana ndoto ya kumiliki kiwanda kikubwa kinachoweza kutengeneza na kufikisha ashkrimu kwa Tanzania na Afrika Mashariki ifikapo mwaka 2020.
Akiwa ameanza kazi hiyo mwaka 2010 kutoka ‘jiko’ la nyumbani Mercy amefanikiwa kutambua wigo wake wa biashara ambayo amesema ina changamoto nyingi hasa mifumo ya vibali na ulipaji kodi na ushuru.















Mjasiriamali kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari wakati akizungumza na Meneja Uendeshaji wa mtandao wa Habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige (hayupo pichani)
























Muonekano wa nje wa duka la Ice Cream la Nelwa’s Gelato lililopo ndani ya Petrol Station ya SOPCO barabara ya Morogoro-Magomeni Mwembechai karibu na kwa Sheikh Yahya.
Alisema uwapo wa kodi nyingi zenye viwango sawa kati ya anayeanza na aliyekuwepo; anayeingiza kidogo na kikubwa kunaleta athari kubwa kwa wajasiriamali wanaotaka kuchomoza.
“To be honest (nikiwa mkweli) zinavunja moyo… nyingi zinakwamisha kwani sisi waelewe tu kwamba tunatengeneza ajira na tunatengeneza soko kama mimi nanunua matunda natengeneza soko la mkulima.,.. natengeneza ashkrimu (Ice Cream) natengeneza ajira.. ipo haja ya kuangalia mambo mengi na hasa hili la kodi na ushuru” alisema.
Alisema ana mambo mengi ya kumwambia Rais Magufuli kama mjasiriamali mwanamke kijana.
“Atupe nafasi tukutane naye wanawake wajasiriamali vijana kisha tutamweleza mengi yakiwemo ya kodi na mifumo yake, mimi ningemweleza haja ya vyombo vyote vya huduma kutumia mtandao, kutoa huduma ,ningemweleza haja ya halmashauri na taasisi kutoa mafunzo mbalimbali ili kuinua wajasiriamali hawa na kuwasapoti si tu kuchukua kodi na ushuru” anasema Mercy.
Anasema wajasiriamali wengi wadogo hawaendelei kwa kukosa sapoti ya mafunzo na namna ya kufanya biashara zao zikue.
“Wasiwe wanachukua kodi na ushuru tu, halmashauri hizi lazima zianze kufikiria kukuza wajasiriamali kwa kuwapa elimu inayostahili katika biashara zao” anasisisitiza Mercy ambaye amesema angelipenda kumuona Role Model wake (Rais Magufuli) kumweleza mengi yanayohusu wanawake vijana na viwanda vidogo kuelekea viwanda vikubwa na hamu ya wajasiriamali wanawake vijana kuchangia pato la taifa na kulipa heshima.
Anasema anapokutana na wajasiriamali wa Uganda, Rwanda anaona jinsi serikali zao zinavyowasaidia kunyanyuka na anaona serikali ya awamu ya tano inaweza kuwasikia na wao wakanyanyuka.

WACHINA WAKOMBOA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU TANZANIA

DAR ES SALAAM

Katika kuimarisha ushirikiano baina ya serikali ya Tanzania na China makampuni zaidi ya 100 yanatarajiwa kukutana na wanafunzi wa elimu ya juu ambapo mkusanyiko wa Kampuni hizo ni moja ya juhudi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Confucius ya Chuo hicho na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China Tanzania za kupunguza tatizo la ajira kwa wahitimu watarajiwa.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho Upande wa Taaluma, Prof. Florence Luhoga, alisema wameamua kuwakutanisha wawekezaji hao na wanafunzi na wahitimu watarajiwa wa vyuo vikuu mbalimbali Tanzania ili kuweza kubaini wenyewe mahitaji yao ya wafanyakazi wazawa.

“Hii ni fursa kwa Watanzania hasa wale wahitimu watarajiwa kwenye vyuo vyetu, lakini pia nifursa kwa wanafunzi hivyo ni muhimu siku hiyo wakaja na vyeti vyao halisi na CV zao, kwasababu kutakuwa na kampuni zitakazowafanyia usaili papohapo.” alisema Luhoga.

Hii ni mara ya kwanza kuandaliwa kwa mkusanyiko huo na unatarajiwa kutoa fursa kubwa ya ajira za ndani ya nchi na China kwa watakao fuzu kwenye usaili.

Aidha Luhoga alivitaja vyuo vinavyoshiriki moja kwa moja kwenye maenyesho hayo ya kazi za kampuni kuwa ni, Mwalimu K.Nyerere Campass ya Dar es Salaam, Chuo Kiuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Campass ya Elimu (DUCE), Chuo cha Mkwawa (MUSE) na Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST), Chuo Kikuu cha St.Augostine (SAUTI), Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Chuo Kikuu cha Dodoma.Maonyesho hayo ya kazi za kampuni yanatarajiwa kujikita katika taaluma za Biashara, Rasiimali Watu, Mauzo, Utunzaji wa Kumbuumbu, Uongozi Katika Biashara, Uhandisi wa aina mbalimbali na fani zingine mbalimbali, Lengo la maonyesho hayo ni kuwanufaisha wahitimu moja kwa moja na fursa za ajira kwa kampuni pamoja na kupunguza tatizo la ajira.