Ijumaa, 17 Juni 2016

SERIKALI YAONGEZA MUDA KWENYE MADUKA MAKUBWA DAR ES SALAAM

DAR ES SALAAM
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam inakusudia kuruhusu baadhi ya maduka makubwa kutoa huduma zaidi ya muda wa kawaida wa maduka kufungwa ili kutoa fursa kwa wafanyakazi kupata huduma hiyo pindi wanapotoka makazini.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda  alipomwakilisha Makamu wa Rais kwenye hafla ya Futali iliyoandaliwa na Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam.
Makonda alisema kuwa kusudio hilo linatokana na changamoto ya upatikanaji wa nafasi ya kupata huduma hiyo kwa wafanyakazi  kwani uchelewa kutoka maofisini jambo lilalosababisha baadhi ya wafanyabiashara kupeleka bidhaa zao huko huko ofisini.
Aliongeza kuwa amekusudia kufanya mambo muhimu matatu katika kipindi hiki cha mwenzi mtukufu wa ramadhani ambapo aliyataja mambo hayo kuwa ni kuongeza muda wa kufunga maduka hasa yale makubwa (malls), kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma na kupambana na watumiaji wa usafiri wa pikipiki wanaokiuka sheria ya matumizi ya Kofia ngumu (helmet).
“Nimekusudia kufanya mambo muhimu matatu ndani ya mwezi huu mtukufu wa ramadhan, niwadokeze tu kuwa mambo hayo ni pamoja na kuongeza muda wa kufanya biashara kwa maduka makubwa (shopping malls), kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma na kupambana na wavunjifu wa sheria ya matumizi ya helmet.” Alisema Makonda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania Bibi. Ineke Bussemaker alisema kuwa wao kama Taasisi ya Kifedha imekuwa na desturi ya kuwajali wateja wao hivyo wanatumia fursa hii kushiriki pamoja na wateja wao walio katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kuwatia moyo wakustahilifunga hiyo muhimu katika uislamu.
Aidha aliongeza kuwa NMB itaendelea kushirikiana na jamii mbalimbali katika kuhakikisha inasaidia pale panapohitajika msaada wao kama ambavyo wamekuwa wakitoa misaada katika kuchangia huduma za kijamii kama vile madawati.

p.txt

MJASILIAMALI MERCY KITOMARY ANATAMANI KUKUTANA NA RAISI MAGUFULI

DAR ES SALAAM

MJASIRIAMALI kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari amesema anatamani kukutana na Rais John Pombe Magufuli kumwelezea haja ya kukutana na wanawake wajasiriamali vijana wamweleze matatizo yao.
Amesema Rais baada ya kukutana na makundi mbalimbali ya wafanyabiashara , inafaa akutane na wajasiriamali wanawake vijana ambao wanapita katika magumu mbalimbali .
Alisema katika mahojiano hivi karibuni ambayo sehemu yake itachapishwa katika mtandao wa Modewjiblog muda wowote kwamba, rais Magufuli akiwa kama ‘Role Model wake’ katika kujituma, anaweza kuwasikiliza wanawake hao vijana na kusaidia kuwasukuma juu zaidi katika kampeni ya kuiweka Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
“Nimekuwa nikikutana na wanawake wenzangu ambao wamekata tamaa na wamekuwa wakiniuliza ninawezaje kuendelea, nikawambia wasi-give up (wasikate tama) na kwamba serikali hii ni ya viwanda na kuchapa kazi “ alisema na kufafanua kwamba wanachohitaji wanawake hao ni mazingira mazuri ya kufanya ujasiriamali.
Mercy ambaye anatengeneza ‘ice cream’ zinazotumia matunda yote ya kitanzania kama vile fenesi, nanasi, bungo, ndizi, embe ana ndoto ya kumiliki kiwanda kikubwa kinachoweza kutengeneza na kufikisha ashkrimu kwa Tanzania na Afrika Mashariki ifikapo mwaka 2020.
Akiwa ameanza kazi hiyo mwaka 2010 kutoka ‘jiko’ la nyumbani Mercy amefanikiwa kutambua wigo wake wa biashara ambayo amesema ina changamoto nyingi hasa mifumo ya vibali na ulipaji kodi na ushuru.















Mjasiriamali kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari wakati akizungumza na Meneja Uendeshaji wa mtandao wa Habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige (hayupo pichani)
























Muonekano wa nje wa duka la Ice Cream la Nelwa’s Gelato lililopo ndani ya Petrol Station ya SOPCO barabara ya Morogoro-Magomeni Mwembechai karibu na kwa Sheikh Yahya.
Alisema uwapo wa kodi nyingi zenye viwango sawa kati ya anayeanza na aliyekuwepo; anayeingiza kidogo na kikubwa kunaleta athari kubwa kwa wajasiriamali wanaotaka kuchomoza.
“To be honest (nikiwa mkweli) zinavunja moyo… nyingi zinakwamisha kwani sisi waelewe tu kwamba tunatengeneza ajira na tunatengeneza soko kama mimi nanunua matunda natengeneza soko la mkulima.,.. natengeneza ashkrimu (Ice Cream) natengeneza ajira.. ipo haja ya kuangalia mambo mengi na hasa hili la kodi na ushuru” alisema.
Alisema ana mambo mengi ya kumwambia Rais Magufuli kama mjasiriamali mwanamke kijana.
“Atupe nafasi tukutane naye wanawake wajasiriamali vijana kisha tutamweleza mengi yakiwemo ya kodi na mifumo yake, mimi ningemweleza haja ya vyombo vyote vya huduma kutumia mtandao, kutoa huduma ,ningemweleza haja ya halmashauri na taasisi kutoa mafunzo mbalimbali ili kuinua wajasiriamali hawa na kuwasapoti si tu kuchukua kodi na ushuru” anasema Mercy.
Anasema wajasiriamali wengi wadogo hawaendelei kwa kukosa sapoti ya mafunzo na namna ya kufanya biashara zao zikue.
“Wasiwe wanachukua kodi na ushuru tu, halmashauri hizi lazima zianze kufikiria kukuza wajasiriamali kwa kuwapa elimu inayostahili katika biashara zao” anasisisitiza Mercy ambaye amesema angelipenda kumuona Role Model wake (Rais Magufuli) kumweleza mengi yanayohusu wanawake vijana na viwanda vidogo kuelekea viwanda vikubwa na hamu ya wajasiriamali wanawake vijana kuchangia pato la taifa na kulipa heshima.
Anasema anapokutana na wajasiriamali wa Uganda, Rwanda anaona jinsi serikali zao zinavyowasaidia kunyanyuka na anaona serikali ya awamu ya tano inaweza kuwasikia na wao wakanyanyuka.

WACHINA WAKOMBOA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU TANZANIA

DAR ES SALAAM

Katika kuimarisha ushirikiano baina ya serikali ya Tanzania na China makampuni zaidi ya 100 yanatarajiwa kukutana na wanafunzi wa elimu ya juu ambapo mkusanyiko wa Kampuni hizo ni moja ya juhudi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Confucius ya Chuo hicho na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China Tanzania za kupunguza tatizo la ajira kwa wahitimu watarajiwa.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho Upande wa Taaluma, Prof. Florence Luhoga, alisema wameamua kuwakutanisha wawekezaji hao na wanafunzi na wahitimu watarajiwa wa vyuo vikuu mbalimbali Tanzania ili kuweza kubaini wenyewe mahitaji yao ya wafanyakazi wazawa.

“Hii ni fursa kwa Watanzania hasa wale wahitimu watarajiwa kwenye vyuo vyetu, lakini pia nifursa kwa wanafunzi hivyo ni muhimu siku hiyo wakaja na vyeti vyao halisi na CV zao, kwasababu kutakuwa na kampuni zitakazowafanyia usaili papohapo.” alisema Luhoga.

Hii ni mara ya kwanza kuandaliwa kwa mkusanyiko huo na unatarajiwa kutoa fursa kubwa ya ajira za ndani ya nchi na China kwa watakao fuzu kwenye usaili.

Aidha Luhoga alivitaja vyuo vinavyoshiriki moja kwa moja kwenye maenyesho hayo ya kazi za kampuni kuwa ni, Mwalimu K.Nyerere Campass ya Dar es Salaam, Chuo Kiuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Campass ya Elimu (DUCE), Chuo cha Mkwawa (MUSE) na Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST), Chuo Kikuu cha St.Augostine (SAUTI), Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Chuo Kikuu cha Dodoma.Maonyesho hayo ya kazi za kampuni yanatarajiwa kujikita katika taaluma za Biashara, Rasiimali Watu, Mauzo, Utunzaji wa Kumbuumbu, Uongozi Katika Biashara, Uhandisi wa aina mbalimbali na fani zingine mbalimbali, Lengo la maonyesho hayo ni kuwanufaisha wahitimu moja kwa moja na fursa za ajira kwa kampuni pamoja na kupunguza tatizo la ajira.

Jumatatu, 30 Mei 2016

19 WATAJWA KUSHIRIKI SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA MSIMU WA TANO 2016

Hatimaye 19 watajwa kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa tano kwa mwaka huu 2016, ambapo fomu 3000 zilizotumwa na wakulima wanawake kote nchini, fomu 1795 zilipitiwa na kuwapata washiriki hao ambao wataanza kutembelewa mmoja mmoja ili kuhakiki iwapo kile walichokijaza kwenye fomu kinaoana na hali halisi. Mashindano ya Mama Shujaa wa Chakula 2016, linatarajiwa kufanyika katika kijiji cha Enguiki kilichopo Monduli mkoani Arusha, kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 16 na kurushwa katika Runinga ya ITV.

Akizungumza wakati wa kutangaza majina hayo, mmoja wa majaji wa shindano hilo Jacob Stephen ‘JB’ ambaye ni muigizaji maarufu wa Filamu Tanzania alisema katika uchambuzi wa fomu hizo walikuwa ni wanawake wakulima ambao wanaelimu ya juu na baadhi ya viongozi wa kisiasa na wale wadogo wadogo. 
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster alisema shindano hilo limeanza kuendeshwa kuanzia mwaka 2011 na sasa ni msimu wa tano na limefanikiwa kuwaunganisha wanawake wakulima wadogo wadogo ambao ni asilimia 70 ya wanawake nchini. Alisema majaji wamefanya kazi ya kuchambua fomu hizo na kuwapata washiriki ambao watakuwa mabalozi wa kuwasilishwa matakwa yao ili changamoto zilizopo zitatuliwe. 
Alisema majaji wamefanya kazi ya kuchambua fomu hizo na kuwapata washiriki ambao watakuwa mabalozi wa kuwasilishwa matakwa yao ili changamoto zilizopo zitatuliwe. Aliongeza kuwa shindano la mama shujaa wa Chakula linaendeshwa katika nchi tatu Afrika ikiwemo Nigeria, Ethiopia na Tanzania. Ambapo Tanzania wamepita katika mikoa mbalimbali na kukusanya wanawake wakulima wadogo wadogo ambao tunaamini kwa kuwa pamoja wanaweza kupaza sauti kwa watunga sera kuhusu changamoto wanazokutana nazo. 
Afisa Uhakiki wa Ubora TBS, Stela Mroso alisema shirika la viwango nchini liliungana na Oxfam mwaka jana ili kuhakikisha wanawaleta wanawake pamoja na kutoa elimu zaidi kuhusu kilimo chenye ubora na mazao yanayoweza kuwa na viwango vya kimataifa. Alisema bila viwango wanawake hawawezi kufanya biashara, huku akitoa wito kwao kujitokeza ili kuangalia ubora wa mazao wanayozalisha. Aliongeza kuwa asilimia 80 ya wanawake nchini wanajishughulisha na Kilimo kwa hiyo ni muhimu chakula kinachozalishwa kiwe katika ubora na afya pia kiweze kuzaliswa Kimataifa. 
Washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula 2016 kuwa ni Betty Nyange (62) Mkoa wa Morogoro, Monica Charles Mduwile (44) Mkoa wa Dodoma, Neema Gilbet Uhagile (29) Mkoa wa Njombe, Mary Christopher Lyatuu (29) Mkoa wa Arusha, Loyce Daudi Mazengo (39) Mkoa wa Singida, Anjela Chogsasi Mswete (48) Mkoa wa Iringa, Lucina Sylivester Assey (54) Mkoa wa Shinyanga, Marta Massesa Nyalama (50) Mkoa wa Kaskazini Unguja, Christina Machumu (42) Mkoa wa Mara, Happiness Paulo Raulent (35) Mkoa wa Kagera. Mary Bony Soko (42) Mkoa wa Ruvuma, Mary Ramadhani Mwiru (39) Mkoa wa Kilimanjaro, Mwanaid Alli Abdalla (53) Mkoa wa Mjini Magharibi, Maria Alfred Mbuya (43) Mkoa wa Mbeya, Eliza Richard Mwansasu (30) Mkoa wa Rukwa, Mwajibu Hasani Binamu (46) Mkoa wa Mtwara, Eva Haprisoni Sikaponda (40) Mkoa wa Songwe, Hidaya Said Musa (40) Mkoa wa Tanga na Mwasiti Salim Mazuri (40) Mkoa wa Dar es salaam Wilaya ya Kinondoni.



Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster(aliyesimama) akiwapongeza washiriki wote waliojaza fomu za kushiriki shindano la mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016 kutoka mikoa mbalimbali nchini. 
Meneja utetezi kutoka Oxfam Tanzania Eluka Kibona akitoa maelezo kuhusu Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kuwa linaendeshwa Tanzania,Nigeria na Ethiopia ambapo alisema lengo la shindano ni kutambua mchango wa wanawake katika mapambano dhidi ya umasikini na kuleta uhakika wa chakula.
Afisa uhakiki wa ubora kutoka TBS Stela Mroso akisisitiza jambo kuhusu ushirikiano wao kama Shirika la Viwango la TBS na Oxfam Tanzania kuhakikisha wanatetea wanawake.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo Paskarina Kayuma akitoa Shukurani kwa Shirika la Oxfam Tanzania kwa kuendelea kuwanyanyua wanawake katika kilimo na amewaomba juhudi hizo ziendelee.
Miongoni mwa majaji Edna Kiogwe mshiriki wa mama Shujaa wa Chakula msimu uliopita(Kulia) pamoja na Fredy Njeje kutoka Blogs za Mikoa (Kushoto) wakielezea namna usaili ulivyofanyika mpaka kuwapata washiriki 19 katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu wa tano kwa mwaka 2016.
Aliyekuwa mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu uliopita Ester Kulwa akionesha kanda zote ambazo washiriki wametokea.
Mabalozi wa Chakula na Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Shirika la Oxfam kwa upande wa Tanzania Shamim Mwasha ambaye pia ni Fashion Blogger(wa kwanza kushoto), Jacob Stephen 'JB' Msanii Maarufu wa Bongo Movie(wa katikati) na Khadija Mwanamboka wakitangaza majina 19 ya washiriki wa shindano la Mama shujaa wa chakula 2016 msimu wa tano.
Baadhi ya wageni wakiwa katika Hafla fupi ya kutangaza majina 19 ya washiriki katika shindano la Mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016.
Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kutoka Morogoro Caroline Chelele akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Aliyekuwa Mshiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Pili Kashinje akizungumza jambo wakati wa Hafla fupi ya kutangaza washiriki shindano la Mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016.
Suhaila Thawer ambaye ni 'Public Forum Officer' kutoka Shirika la Oxfam Tanzania akitoa neno la Shukurani.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Majaji,Wafanyakazi wa Oxfam pamoja na Mabalozi wa Chakula na Kampeni ya Grow.
Waliosaidia katika kupitia Fomu za Mama shujaa wa Chakula kwa hatua ya Mwanzo kutoka Taasisi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster (wa saba kutoka kulia).


Jumatano, 18 Mei 2016

NSSF YATOA ELIMU KUHUSU HIFADHI YA JAMII KWA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA.

SHIRIKA la  Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) yazidi kutoa elimu juu ya hifahdi ya jamii kwa wananchi mbalimbali ikiwa ni  mpango maalamu wa kuwafikia wanachama  wengi zaidi.
Katika mkoa wa Arusha NSSF imetoa elimu kwa wafanyabiashara wadogowadogo katika soko la Kilombero.Zoezi hilo litaendelea kesho tarehe 19/05 katika eneo la soko la Kilombero.
Afisa Masoko na Uhusiano  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Amani Marcel (kushoto), akimkabidhi mwanachama mpya fulana wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi iliyofanyika katika Soko la Kilombero Jijini Arusha. 
Wananchi wakiwa katika foleni ya kujiandikisha uanchama wa NSSF wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi iliyofanyika katika Soko la Kilombero jijini Arusha.
Afisa wa NSSF Bi. Irene Mshanga akimwandikisha mwanachama Mpya wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi inayoendelea katika soko la Kilombero jijini Arusha.


Jumanne, 17 Mei 2016

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE ATOA POLE KWA FAMILIA YA DIWANI WA KIJICHI,ANDERSON CHALE ALIYEFARIKI JUZI KWA MSHITUKO WA MOYO

Aidha binamu wa Marehemu aitwaye Anna Komba,alisema kuwa Marehemu Diwani wa Kata ya Kijichi,Anderson Chale alipatwa na mshituko wa moyo kwa taarifa ya hospitali kwa kuwa kabla ya hapo awali alikuwa ana tatizo la Presha na ratiba ya mazishi ni kwamba mwili wa marehemu utasafirishwa jumatano kuelekea nyumbani kwao Liuri,Wilaya ya Nyasa,mkoani Ruvuma kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

 Baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu wakiwa nyumbani kwake kijichi ambako msiba ulipo.

 Mkuu wa Polisi Mkoa wa Temeke,RPC Kamishina Msaidizi, Gilles Muroto,akisalimiana na Aliyekuwa Diwani wa Kurasini (CCM),Wilfred Kimath baada ya kuongozana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Sophia Mjema (katikati) kwenda kutoa pole nyumbani kwa marehemu.



 Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Sophia Mjema,akisikiliza kutoka kwa ndugu wa marehemu chanzo cha msiba wa marehem,u ambacho ni mshituko wa moyo.



 Wakazi wa eneo hilo wakiomboleza

 Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa kwenye msiba huo



Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Sophia Mjema,akitoa pole kwa ndugu wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kijichi CCM,Anderson Chale,aliyefariki dunia juzi kwa mshituko wa moyo,nyumbani kwake,Kijichi,jijini Dar es Salaam,leo. Picha zote na Elisa Shunda

 Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika msiba huo nyumbani kwa marehemu kijichi

 Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Sophia Mjema  na msafara wake wakiondoka katika eneo hilo baada ya kutoa pole kutoka ofisi ya Wilaya ya Temeke.

Muonekano wa Nyumba ya Marehemu aliyokuwa akiishi eneo la Kijichi,wilayani Temeke,Dar es Salaam
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina Lake Lihimidiwe

Ijumaa, 13 Mei 2016

WANAOTUMIA MIILI YAO KUJIUZA 52 WAMEKAMATWA











Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi,akizungumza na waandishi wa habari,Dar es Salaam, jana kuhusu kubainika watumishi hewa wengine 14 na kupanga mkakati wa kusafisha wilaya hiyo. Picha na Elisa Shunda.

DAR ES SALAAM,
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, amesema jumla ya watumishi hewa 16 kati ya 103 wamerudisha zaidi ya Sh. Milioni 94 huku kukiwa na hasara ya takriban Sh. Bilioni moja iliyopotea.
Imeelezwa kuwa watumishi hao kwa sasa wako nje kwa dhamana huku msako wa kuwatafuta wengine ukiendelea ili fedha zilizopotea ziweze kurudishwa pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa waliohusika.
Hapi alisema hayo jana jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mambo kadhaa yakiwemo operesheni ya safisha kinondoni pamoja na sakata la watumishi hewa.
Alisema watumishi hao waliorejesha fedha hizo walikamatwa mapema tangu lilipotolewa agizo la kuwasaka watumishi hewa walioisababishia serikali kupoteza kiasi kikubwa cha fedha.
“Watumishi hao waliorudisha fedha hizo ni kutoka idara tofauti za manispaa hii, pia tayari tushawapatia polisi orodha yote ya watumishi hewa ambao hadi sasa wanaendelea kutafutwa na vyombo vya ulinzi na usalama,”alisema.
Akizungumzia operesheni ya safisha kinondoni, alisema vyombo husika vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya misako ikiwemo ya ukwepaji kodi, kufanya biashara bila leseni, machangudoa, madangulo, wazurulaji, magenge ya wahalifu (panyaroad), na mengineyo.
Alisema katika operesheni hiyo, tayari wameshawakamata machangudoa 52, wapiga debe saba na wazurulaji 10 ambao wote kwa pamoja tayari washafikishwa mahakamani.
Hapi amewaonya wamiliki wa bilabu vya pombe (bar) kutojihusisha na biashara haramu ya machangudoa ambapo aliongeza kuwa, hatasita kufungia vilabu vyao iwapo vikibainika.
“Tutapita maeneo yote ya madangulo na vilabu, tutahakikisha biashara hiyo haramu inakoma mara moja na hatutasita kuchukua hatua kwa wataokaidi, lazima utii wa sheria bila shuruti uzingatiwe,”alisema.
Wakati huhuo, Hapi alisema wamelifungia godauni moja lililopo manzese ambalo lilikutwa na bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko 242 ya sukari.
Akielezea sababu za kufungwa kwa godauni hilo, alisema ni kutokana na mmiliki wake, Method John, kutokuwa na leseni ya biashara ambapo kufuatia hatua hiyo ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) tawi la Kinondoni kufanya ukaguzi ili kubaini kiasi cha mapato kilichopotea.
Amewashauri wananchi kutosita katika kutoa usirikiano pindi wanapobaini uhalifu wowote au kuwa na mashaka na mambo fulani ili hatua kadhaa zichukuliwe kwa ajili ya kuinua uchumi wa manispaa hiyo pamoja na kuimarisha hali ya usalama.