Jumatatu, 30 Mei 2016

19 WATAJWA KUSHIRIKI SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA MSIMU WA TANO 2016

Hatimaye 19 watajwa kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa tano kwa mwaka huu 2016, ambapo fomu 3000 zilizotumwa na wakulima wanawake kote nchini, fomu 1795 zilipitiwa na kuwapata washiriki hao ambao wataanza kutembelewa mmoja mmoja ili kuhakiki iwapo kile walichokijaza kwenye fomu kinaoana na hali halisi. Mashindano ya Mama Shujaa wa Chakula 2016, linatarajiwa kufanyika katika kijiji cha Enguiki kilichopo Monduli mkoani Arusha, kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 16 na kurushwa katika Runinga ya ITV.

Akizungumza wakati wa kutangaza majina hayo, mmoja wa majaji wa shindano hilo Jacob Stephen ‘JB’ ambaye ni muigizaji maarufu wa Filamu Tanzania alisema katika uchambuzi wa fomu hizo walikuwa ni wanawake wakulima ambao wanaelimu ya juu na baadhi ya viongozi wa kisiasa na wale wadogo wadogo. 
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster alisema shindano hilo limeanza kuendeshwa kuanzia mwaka 2011 na sasa ni msimu wa tano na limefanikiwa kuwaunganisha wanawake wakulima wadogo wadogo ambao ni asilimia 70 ya wanawake nchini. Alisema majaji wamefanya kazi ya kuchambua fomu hizo na kuwapata washiriki ambao watakuwa mabalozi wa kuwasilishwa matakwa yao ili changamoto zilizopo zitatuliwe. 
Alisema majaji wamefanya kazi ya kuchambua fomu hizo na kuwapata washiriki ambao watakuwa mabalozi wa kuwasilishwa matakwa yao ili changamoto zilizopo zitatuliwe. Aliongeza kuwa shindano la mama shujaa wa Chakula linaendeshwa katika nchi tatu Afrika ikiwemo Nigeria, Ethiopia na Tanzania. Ambapo Tanzania wamepita katika mikoa mbalimbali na kukusanya wanawake wakulima wadogo wadogo ambao tunaamini kwa kuwa pamoja wanaweza kupaza sauti kwa watunga sera kuhusu changamoto wanazokutana nazo. 
Afisa Uhakiki wa Ubora TBS, Stela Mroso alisema shirika la viwango nchini liliungana na Oxfam mwaka jana ili kuhakikisha wanawaleta wanawake pamoja na kutoa elimu zaidi kuhusu kilimo chenye ubora na mazao yanayoweza kuwa na viwango vya kimataifa. Alisema bila viwango wanawake hawawezi kufanya biashara, huku akitoa wito kwao kujitokeza ili kuangalia ubora wa mazao wanayozalisha. Aliongeza kuwa asilimia 80 ya wanawake nchini wanajishughulisha na Kilimo kwa hiyo ni muhimu chakula kinachozalishwa kiwe katika ubora na afya pia kiweze kuzaliswa Kimataifa. 
Washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula 2016 kuwa ni Betty Nyange (62) Mkoa wa Morogoro, Monica Charles Mduwile (44) Mkoa wa Dodoma, Neema Gilbet Uhagile (29) Mkoa wa Njombe, Mary Christopher Lyatuu (29) Mkoa wa Arusha, Loyce Daudi Mazengo (39) Mkoa wa Singida, Anjela Chogsasi Mswete (48) Mkoa wa Iringa, Lucina Sylivester Assey (54) Mkoa wa Shinyanga, Marta Massesa Nyalama (50) Mkoa wa Kaskazini Unguja, Christina Machumu (42) Mkoa wa Mara, Happiness Paulo Raulent (35) Mkoa wa Kagera. Mary Bony Soko (42) Mkoa wa Ruvuma, Mary Ramadhani Mwiru (39) Mkoa wa Kilimanjaro, Mwanaid Alli Abdalla (53) Mkoa wa Mjini Magharibi, Maria Alfred Mbuya (43) Mkoa wa Mbeya, Eliza Richard Mwansasu (30) Mkoa wa Rukwa, Mwajibu Hasani Binamu (46) Mkoa wa Mtwara, Eva Haprisoni Sikaponda (40) Mkoa wa Songwe, Hidaya Said Musa (40) Mkoa wa Tanga na Mwasiti Salim Mazuri (40) Mkoa wa Dar es salaam Wilaya ya Kinondoni.



Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster(aliyesimama) akiwapongeza washiriki wote waliojaza fomu za kushiriki shindano la mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016 kutoka mikoa mbalimbali nchini. 
Meneja utetezi kutoka Oxfam Tanzania Eluka Kibona akitoa maelezo kuhusu Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kuwa linaendeshwa Tanzania,Nigeria na Ethiopia ambapo alisema lengo la shindano ni kutambua mchango wa wanawake katika mapambano dhidi ya umasikini na kuleta uhakika wa chakula.
Afisa uhakiki wa ubora kutoka TBS Stela Mroso akisisitiza jambo kuhusu ushirikiano wao kama Shirika la Viwango la TBS na Oxfam Tanzania kuhakikisha wanatetea wanawake.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo Paskarina Kayuma akitoa Shukurani kwa Shirika la Oxfam Tanzania kwa kuendelea kuwanyanyua wanawake katika kilimo na amewaomba juhudi hizo ziendelee.
Miongoni mwa majaji Edna Kiogwe mshiriki wa mama Shujaa wa Chakula msimu uliopita(Kulia) pamoja na Fredy Njeje kutoka Blogs za Mikoa (Kushoto) wakielezea namna usaili ulivyofanyika mpaka kuwapata washiriki 19 katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu wa tano kwa mwaka 2016.
Aliyekuwa mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu uliopita Ester Kulwa akionesha kanda zote ambazo washiriki wametokea.
Mabalozi wa Chakula na Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Shirika la Oxfam kwa upande wa Tanzania Shamim Mwasha ambaye pia ni Fashion Blogger(wa kwanza kushoto), Jacob Stephen 'JB' Msanii Maarufu wa Bongo Movie(wa katikati) na Khadija Mwanamboka wakitangaza majina 19 ya washiriki wa shindano la Mama shujaa wa chakula 2016 msimu wa tano.
Baadhi ya wageni wakiwa katika Hafla fupi ya kutangaza majina 19 ya washiriki katika shindano la Mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016.
Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kutoka Morogoro Caroline Chelele akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Aliyekuwa Mshiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Pili Kashinje akizungumza jambo wakati wa Hafla fupi ya kutangaza washiriki shindano la Mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016.
Suhaila Thawer ambaye ni 'Public Forum Officer' kutoka Shirika la Oxfam Tanzania akitoa neno la Shukurani.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Majaji,Wafanyakazi wa Oxfam pamoja na Mabalozi wa Chakula na Kampeni ya Grow.
Waliosaidia katika kupitia Fomu za Mama shujaa wa Chakula kwa hatua ya Mwanzo kutoka Taasisi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster (wa saba kutoka kulia).


Jumatano, 18 Mei 2016

NSSF YATOA ELIMU KUHUSU HIFADHI YA JAMII KWA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA.

SHIRIKA la  Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) yazidi kutoa elimu juu ya hifahdi ya jamii kwa wananchi mbalimbali ikiwa ni  mpango maalamu wa kuwafikia wanachama  wengi zaidi.
Katika mkoa wa Arusha NSSF imetoa elimu kwa wafanyabiashara wadogowadogo katika soko la Kilombero.Zoezi hilo litaendelea kesho tarehe 19/05 katika eneo la soko la Kilombero.
Afisa Masoko na Uhusiano  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Amani Marcel (kushoto), akimkabidhi mwanachama mpya fulana wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi iliyofanyika katika Soko la Kilombero Jijini Arusha. 
Wananchi wakiwa katika foleni ya kujiandikisha uanchama wa NSSF wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi iliyofanyika katika Soko la Kilombero jijini Arusha.
Afisa wa NSSF Bi. Irene Mshanga akimwandikisha mwanachama Mpya wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi inayoendelea katika soko la Kilombero jijini Arusha.


Jumanne, 17 Mei 2016

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE ATOA POLE KWA FAMILIA YA DIWANI WA KIJICHI,ANDERSON CHALE ALIYEFARIKI JUZI KWA MSHITUKO WA MOYO

Aidha binamu wa Marehemu aitwaye Anna Komba,alisema kuwa Marehemu Diwani wa Kata ya Kijichi,Anderson Chale alipatwa na mshituko wa moyo kwa taarifa ya hospitali kwa kuwa kabla ya hapo awali alikuwa ana tatizo la Presha na ratiba ya mazishi ni kwamba mwili wa marehemu utasafirishwa jumatano kuelekea nyumbani kwao Liuri,Wilaya ya Nyasa,mkoani Ruvuma kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

 Baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu wakiwa nyumbani kwake kijichi ambako msiba ulipo.

 Mkuu wa Polisi Mkoa wa Temeke,RPC Kamishina Msaidizi, Gilles Muroto,akisalimiana na Aliyekuwa Diwani wa Kurasini (CCM),Wilfred Kimath baada ya kuongozana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Sophia Mjema (katikati) kwenda kutoa pole nyumbani kwa marehemu.



 Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Sophia Mjema,akisikiliza kutoka kwa ndugu wa marehemu chanzo cha msiba wa marehem,u ambacho ni mshituko wa moyo.



 Wakazi wa eneo hilo wakiomboleza

 Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa kwenye msiba huo



Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Sophia Mjema,akitoa pole kwa ndugu wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kijichi CCM,Anderson Chale,aliyefariki dunia juzi kwa mshituko wa moyo,nyumbani kwake,Kijichi,jijini Dar es Salaam,leo. Picha zote na Elisa Shunda

 Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika msiba huo nyumbani kwa marehemu kijichi

 Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Sophia Mjema  na msafara wake wakiondoka katika eneo hilo baada ya kutoa pole kutoka ofisi ya Wilaya ya Temeke.

Muonekano wa Nyumba ya Marehemu aliyokuwa akiishi eneo la Kijichi,wilayani Temeke,Dar es Salaam
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina Lake Lihimidiwe

Ijumaa, 13 Mei 2016

WANAOTUMIA MIILI YAO KUJIUZA 52 WAMEKAMATWA











Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi,akizungumza na waandishi wa habari,Dar es Salaam, jana kuhusu kubainika watumishi hewa wengine 14 na kupanga mkakati wa kusafisha wilaya hiyo. Picha na Elisa Shunda.

DAR ES SALAAM,
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, amesema jumla ya watumishi hewa 16 kati ya 103 wamerudisha zaidi ya Sh. Milioni 94 huku kukiwa na hasara ya takriban Sh. Bilioni moja iliyopotea.
Imeelezwa kuwa watumishi hao kwa sasa wako nje kwa dhamana huku msako wa kuwatafuta wengine ukiendelea ili fedha zilizopotea ziweze kurudishwa pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa waliohusika.
Hapi alisema hayo jana jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mambo kadhaa yakiwemo operesheni ya safisha kinondoni pamoja na sakata la watumishi hewa.
Alisema watumishi hao waliorejesha fedha hizo walikamatwa mapema tangu lilipotolewa agizo la kuwasaka watumishi hewa walioisababishia serikali kupoteza kiasi kikubwa cha fedha.
“Watumishi hao waliorudisha fedha hizo ni kutoka idara tofauti za manispaa hii, pia tayari tushawapatia polisi orodha yote ya watumishi hewa ambao hadi sasa wanaendelea kutafutwa na vyombo vya ulinzi na usalama,”alisema.
Akizungumzia operesheni ya safisha kinondoni, alisema vyombo husika vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya misako ikiwemo ya ukwepaji kodi, kufanya biashara bila leseni, machangudoa, madangulo, wazurulaji, magenge ya wahalifu (panyaroad), na mengineyo.
Alisema katika operesheni hiyo, tayari wameshawakamata machangudoa 52, wapiga debe saba na wazurulaji 10 ambao wote kwa pamoja tayari washafikishwa mahakamani.
Hapi amewaonya wamiliki wa bilabu vya pombe (bar) kutojihusisha na biashara haramu ya machangudoa ambapo aliongeza kuwa, hatasita kufungia vilabu vyao iwapo vikibainika.
“Tutapita maeneo yote ya madangulo na vilabu, tutahakikisha biashara hiyo haramu inakoma mara moja na hatutasita kuchukua hatua kwa wataokaidi, lazima utii wa sheria bila shuruti uzingatiwe,”alisema.
Wakati huhuo, Hapi alisema wamelifungia godauni moja lililopo manzese ambalo lilikutwa na bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko 242 ya sukari.
Akielezea sababu za kufungwa kwa godauni hilo, alisema ni kutokana na mmiliki wake, Method John, kutokuwa na leseni ya biashara ambapo kufuatia hatua hiyo ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) tawi la Kinondoni kufanya ukaguzi ili kubaini kiasi cha mapato kilichopotea.
Amewashauri wananchi kutosita katika kutoa usirikiano pindi wanapobaini uhalifu wowote au kuwa na mashaka na mambo fulani ili hatua kadhaa zichukuliwe kwa ajili ya kuinua uchumi wa manispaa hiyo pamoja na kuimarisha hali ya usalama.

MWENGE WA UHURU ZATIMIA

MWENGE WA UHURU WAINGIA MKOA WA MJINI MAGHARIBI BAADA YA KUMALIZA MBIO ZAKE MKOA WA KASKAZINI


 Gari la kukimbiza Mwenge wa Uhuru 2016 likikata viunga vya Kihinani
Wilaya ya Magharibi A. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
 Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Meja Mstafu. Juma Kasim Tindwa akimkabidhi Mwenge
wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis tayari kwa kukimbizwa katika mkoa huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis akimkabidhi Mwenge
wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Mwinyiussi Abdalla kwa ajili ya kukimbizwa katika Wilaya yake.
 Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Mwinyiussi Abdalla akiteta kitu na kiongozi
wa mbio za Mwenge 2016 George Jackson Mbijima wakati wa sherehe za makabidhia
ya Mwenge yaliyofanyika Mfenesini Wilaya ya Magharibi A.
Mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2016 James Sadick Munguji akiongoza
mbio hizo katika mitaa ya Mfenesini,
Wilaya ya Magharibi A.

WASANII LIVE BUNGENI LEO

MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA UWASILISHWAJI WA BAJETI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO BUNGENI MJINI DODOMA.


 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Mrisho (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Zamaradi Kawawa wakiwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajli ya kusikiliza Bajeti ya Wizara hiyo leo 13 Mei, 2016.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (Mb) (kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya usomwaji wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, 13 Mei, 2016.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (Mb) (kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki wakiwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya usomwaji wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, 13 Mei, 2016.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Profesa Elisante Ole-Gabriel (kulia), Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Mrisho (katikati) pamoja na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN) wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti
ya Wizara hiyo leo 13 Mei, 2016 Bungeni mjini Dodoma.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake Bungeni mjini Dodoma leo 13 Mei,
2016.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Profesa Elisante Ole-Gabriel (katikati), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo, Bi. Zawadi Msalla (kushoto) pamoja na Katibu wa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Bi, Anna Nkinda wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara hiyo leo 13 Mei, 2016 Bungeni mjini Dodoma.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wake, Mhe. Anastazia
Wambura wakijadiliana mara baada ya kuwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni mjini Dodoma leo 13 Mei, 2016.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na Kundi
la Wasanii na Bloggers Bungeni mjini Dodoma 13 Mei, 2016.
 
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO, DODOMA)

Jumatatu, 9 Mei 2016

WANANCHI WAHAMASISHWA KUWEKEZA
























Kaimu Meneja Msaidizi wa Masoko ya Ndani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Genes Gos Kimaro,akifafanua jambo katika mkutano huo.

NA:ELISA SHUNDA,DAR


BENKI kuu ya Tanzania (BOT), imewahamasisha wanachi kutumia soko la dhamana la serikali kwa kuwekeza, na mali zao zitakuwa katika hali ya usalama.
Pia iewataka watu wa Afrika ya Mashariki kuja kuwekeza kupitia dhamana la soko hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko ya fedha, Alexander Ng’winamila, alisema katika uwekezaji huo tasisi nyingi zimeonekana zikitumia dhamana hizo lakini hali ya wananchi imeonekaana kuwa duni.
“Napenda kuwahamasisha wananchi kutumia soko la dhamana la serikali kuwekeza katika dhamana ya muda mfupi na muda mrefu kwani mali zao zitakuwa salama ” alisema Ng’winamila.
Alisema endapo mwananchi atajiunga na soko la dhamana la serikali ataweza kupatiwa mkopo kutokana na dhamana aliyoiweka na kurudisha kidogo kidogo huku akipata fidia.
“Dhamana ya serikali ya muda mfupi ni ukitaka kujiunga ni Sh. 500,000, na dhamana za muda mrefu ni Sh. milioni 1 hadi 50 na hivyo tunawaomba wananchi mjitokeze kuwekeza ili kuweza kujiongezea kipato na maendeleo”alisema.
Meneja Msaidizi masoko ya ndani Genes Kimaro, alisema wananchi anayetaka kujiunga wafike kwa mawakala wao waliopo nchi nzima ili kuweza kufungua account na kuingiziwa kumbukumbu ili kuweza kufikishwa  taarifa zao BOT, kwajili ya kusajiliwa.
Alisema baada ya kusajiliwa kila ijumaa wale wote waliofungua account watapatiwa matangazo ambayo kila jumatano wataweza kushiriki katika mnada wa serikali kupitia soko la dhamana alilojiunga.

AFISA UTUMISHI MANISPAA YA ILALA ASIMAMISHWA KAZI




Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam,Paul Makonda, akizungumza na wakuu wa idara mbalimbali wa mkoa huo kuhusu kubainika kwa watumishi hewa  wengine 39. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi na Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Sophia Mjema. Picha zote na Elisa Shunda 

DAR ES SALAA,
JUMLA ya watumishi hewa wengine 39 wamebainika katika Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni wiki moja tangu Mkuu wa Mkoa wa huo, Paul Makonda, kuwasainisha mikataba wakuu wa idara zote kuhusiana na watumishi hao. 
Imeelezwa kuwa hadi sasa watumishi hewa 248 wamebainika mkoani hapa na kuisababibishia serikali hasara ya takriban Sh.bilioni 3.6. 
Akizungumza na viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo maofisa utumishi, wakuu wa idara, wakurugenzi na wakuu wa wilaya jana jijini hapa, Makonda alisema watumishi hao 39 wameisababishia serikali hasara ya Sh. milioni 724.
Kufuatia sakata hilo, Makonda alimwagiza mkurugenzi wa Ilala, Isaya Mngurumi, kumwandikia barua ya kumsimamisha kazi Ofisa Utumishi wa manispaa hiyo, Francis Kilawe, kutokana na kubainika watumishi hewa 11 ambao licha ya kutoonekana katika idara zao, waliendelea kulipwa mishahara.
Alisema ili taifa liweze kupiga hatua, kila mmoja kwa nafasi aliyonayo hana budi kufanya kazi kwa bidii kumsaidia Rais John Magufuli katika kuhakikisha kuwa maendeleo yanapatikana.
Hata hivyo, akizungumzia suala hilo baada ya mkutano huo kuisha, Mngurumi alisema atamuomba Makonda kutengua adhabu ya ofisa huyo kwani tangu alipowasili kikazi katika manispaa hiyo, haizidi miezi miwili.
“Ofisa huyo ametoka Ilemela na kuja hapa, kwa hiyo nitazungumza na mkuu wa mkoa ili amuondolee adhabu hiyo kwa sababu hana muda mrefu tangu awasili hapa,”alisema.
Makonda alisema amewapa muda wa wiki mbili kwa wakuu hao wa idara kuwasaka watumishi hewa na baada ya hapo, kazi hiyo itakuwa endelevu kwa kila aliyepewa dhamana ya kuisimamia ili kuokoa fedha zilizokuwa zikipotea.
“Haiwezekani mkuu wa idara akae bila ya kufahamu namna ya kuifanya kazi yake hadi alazimishwe au asimamiwe, nataka kuona kila mtu akitekeleza jukumu lake alilopewa kikamilifu,”alisema.
Mkuu huyo wa mkoa alisema serikali imetenga Sh.bilioni 40 kwa ajili ya maendeleo, hivyo bila ya kuwepo na kasi ya utendaji kazi, fedha hizo zinaweza kuliwa na wajanja na hatimaye lengo lisipatikane.
Makonda amewataka viongozi husika kuchukua hatua stahiki dhidi ya watumishi hao ili fedha zilizopotea zirejeshwe pamoja na kufunguliwa mashtaka kwa waliobainika.

WANANCHI WAHAMASISHWA KUJITOKEZA ILI KUPATA MSAADA WA KISHERIA

NA:ELISA SHUNDA,DAR

WIZARA ya Katiba na Sheria, imewataka wananchi wenye uwitaji kupenda kutumia sekretarieti  ya msaada wa kisheria ili kuweza kupata haki zao za msingi.
Ambapo tasisi hiyo ya msaada wa kisheria kwa sasa ipo katika jengo la tasisi ya mafunzo ya uwanasheria kwa vitendo iliyopo Sinza karibu na kituo cha basi cha Mawasiliano.
Imeelezwa kuwa lengo la kutoa tamko hilo imetokaana na wananchi wengi wenye uhitaji kutokupenda  kutimia tasisi zilizopo ili kuweza kusaidiwa kwa kupata msaada wa huduma za kisheria na matokeo yake kudhurumiwa haki zao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Slaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo Shaiba Bulu, alisema watu wengi wanapata matatizo ambayo wananyimwa haki zao za msingi na kushindwa kufungua kesi kwa kuhofia gharama za watetezi wao Mahakamani (Hakimu, Wakili), hivyo wameona ni muhimu kuwahamasisha wananchi kutumia tasisi zilizopo na kupatiwa huduma hizo bure na kupata haki kwa wakati.
“Lengo hasa la huduma hii ni kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake katika mamlaka husika za utoaji haki na wakati”alisema Shaiba.
Alisema sambamba na huduma hiyo kupitia sekretarieti, wizara katika ofisi zake za makao makuu pia imepokea malalamiko ya wananchi yanayohusiana na haki na utoaji wa ushauri na maelekezo ya kufuatilia haki zao.
“Wizara imewafahamisha wananchi kuwa huduma za kisheria kwa watu wenye uhitaji ambao wanakosa huduma za aina hiyo wanaweza kupata huduma hiyo bila malipo ambapo utaratibu huo umefanyika wakati wizara ipo katika hatua ya mwisho ya kutunga sheria ya msaada” alisema.
Alisema mpango huo ulianzishwa mwaka 2012, ili kuwezesha asasi au mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kupanua wigo wa huduma ya msaada wa kisheria kwa wahitaji husuasan wananchi wanaoishi kwenye maeneo ambayo kwa namna moja au nyingine awawezi kupata wala kulipia gharama za mawakili nchini.
Wakili Mkuu wa Serikali Charles Mmbando, aliwaomba mawakili na tasisi zote zinazojishughulisha na hitohaji wa huduma za kisheria nchini kuendelea na utoaji wa huduma hiyo vizuri kwa wananchi wasio na uwezo wa kumudu kulipia gharama za mawakili.
“Nachukua nafasi hii kuwasihi wananchi wasio na uwezo hasa wa maeneo ya vijijini kwenda katika tasisi hizo na nyinginezo ambazo zinatoa  huduma za msaada wa kisheria kama huduma kwa jamii inayozizun guka” alisema Mmbando.


Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Charles Mmbando,akizungumza na waandishi wa habari,Dar es Salaam,jana kuhusu kutumia mpango wa huduma za msaada wa kisheria kupitia sekeretarieti ya msaada wa kisheria na mashirika kwa ajili hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini  kutoka  Wizara hiyo, Shaiba Bulu. Picha na Elisa Shunda




Ijumaa, 6 Mei 2016

DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Issaya Mngurumi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara maeneo yasiyo rasmi hasa barabarani, Amesema kuwa wafanyabiashara hao maalufu kama machinga wanatakiwa kuondoka ifikapo May 8 mwaka huu na kuwa wametafutiwa maeneo kwa ajili ya shughuli za biashara ndogondogo hasa katika maeneo ya Kigogo Fresh, Soko la Tabata Muslimu na eneo lililopo Mkabala na Gereza kuu la Ukonga, Pia amesema kuwa wafanyabiashara ndogondogo watakaohusika ni wale ambao wametambuliwa na kuorodheshwa kutoka maeneo ya Kariakoo, Karume, Buguruni, Ukonga Mombasa, Jangwani, Kibasila, Banana na Gongolamboto.
Mngurumi amesema kuwa wafanyabiashara ndogondogo 2961 wameshatambuliwa na kuorodheshwa  ili waweze kuhamia kwenye maeneo yaliyoandaliwa kwaajili yao.
Wafanyabiashara ndogondogo wamewatakiwa kutekeleza agizo la kuondoka katika maeneo hayo na kwenda maeneo  ambayo watakayogawiwa ifikapo May 8 mwaka huu.

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Issaya Mngurumi,kulia, Afisa Mipango miji mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela(Katikati) na Afisa Afya Halmashauri ya Ilala, Charles Wambura wakiwa katika mkututano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam .
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Alhamisi, 5 Mei 2016

DAR ES SALAAM

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw.BONIFACE JACOB ametangaza kumsimamisha kazi mwanasheria mkuu wa Manispaa hiyo Burton Mahenge na Mthamini wa Manispaa Einhard Chidanga.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema wawili hao wameisababishia hasara kubwa na upotevu wa malikatika manispaa hiyo.
Aidha Bw.Jacob amesema wawili hao wameshtakiwa kwa makosa yafuatayo,Mradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa,Mgogoro wa wapangaji wa nyumba za Magomeni kata,Uwekezaji wa eneo la Coco Beach Oysterbay,Mradi wa ujenzi wa maduka ya Makumbusho,Kubomolewa kwa ofisi ya Kata ya Msasani,Ujenzi wa nyumba za Makazi Hiill Road Oysterbay na Ujenzi wa nyumba za makazi Kiwanja Na.314 Toure Drive.




Jumatano, 4 Mei 2016

DAR ES SALAAM
meelezwa kuwa  asimilia 65 ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani watu wenye albinism wamefanyiwa vitendo vya ukatili  nchini Malawi mwaka 2015.Akizungumza na wanahabari jijini dare s salaam mkurugenzi mkuu wa shirika la under the same sun BW. PETER ASH amesema  kuwa vitendo vya ukatili  kwa watu wenye ulemavu wa ngozi bado  vinaendelea  hivyo kutoa rai kwa serikali kushirikiana na serikali ya Malawi kukabiliana na vitendo hivyo.
Aidha BW.ASH ameushukuru uongozi wa awamu ya tano kwa kumteuwa naibu waziri mwenye  ulemavu wa ngozi akiamini kuwa naibu waziri huyo atasaidia kutetea  haki za watu wenye ulemavu wa ngozi.
















Mkurugenzi Mkuu wa Under the Same Sun Bw.Peter Ash
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa  shirika hilo Tanzania bi. VICKY NTETEMA ametoa wito kwa serikali kuharakisha kutolewa kwa hukumu kwa watu wote watakao bainika  wakifanya vitendo vya ukatili.
Mkurugenzi Msaidizi Tanzania Under the Same Sun Bi.Vicky Ntetema