DAR ES SALAAM
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Issaya Mngurumi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara maeneo yasiyo rasmi hasa barabarani, Amesema kuwa wafanyabiashara hao maalufu kama machinga wanatakiwa kuondoka ifikapo May 8 mwaka huu na kuwa wametafutiwa maeneo kwa ajili ya shughuli za biashara ndogondogo hasa katika maeneo ya Kigogo Fresh, Soko la Tabata Muslimu na eneo lililopo Mkabala na Gereza kuu la Ukonga, Pia amesema kuwa wafanyabiashara ndogondogo watakaohusika ni wale ambao wametambuliwa na kuorodheshwa kutoka maeneo ya Kariakoo, Karume, Buguruni, Ukonga Mombasa, Jangwani, Kibasila, Banana na Gongolamboto.
Mngurumi amesema kuwa wafanyabiashara ndogondogo 2961 wameshatambuliwa na kuorodheshwa ili waweze kuhamia kwenye maeneo yaliyoandaliwa kwaajili yao.
Wafanyabiashara ndogondogo wamewatakiwa kutekeleza agizo la kuondoka katika maeneo hayo na kwenda maeneo ambayo watakayogawiwa ifikapo May 8 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Issaya Mngurumi,kulia, Afisa Mipango miji mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela(Katikati) na Afisa Afya Halmashauri ya Ilala, Charles Wambura wakiwa katika mkututano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam .
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni