Jumatatu, 9 Mei 2016

WANANCHI WAHAMASISHWA KUJITOKEZA ILI KUPATA MSAADA WA KISHERIA

NA:ELISA SHUNDA,DAR

WIZARA ya Katiba na Sheria, imewataka wananchi wenye uwitaji kupenda kutumia sekretarieti  ya msaada wa kisheria ili kuweza kupata haki zao za msingi.
Ambapo tasisi hiyo ya msaada wa kisheria kwa sasa ipo katika jengo la tasisi ya mafunzo ya uwanasheria kwa vitendo iliyopo Sinza karibu na kituo cha basi cha Mawasiliano.
Imeelezwa kuwa lengo la kutoa tamko hilo imetokaana na wananchi wengi wenye uhitaji kutokupenda  kutimia tasisi zilizopo ili kuweza kusaidiwa kwa kupata msaada wa huduma za kisheria na matokeo yake kudhurumiwa haki zao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Slaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo Shaiba Bulu, alisema watu wengi wanapata matatizo ambayo wananyimwa haki zao za msingi na kushindwa kufungua kesi kwa kuhofia gharama za watetezi wao Mahakamani (Hakimu, Wakili), hivyo wameona ni muhimu kuwahamasisha wananchi kutumia tasisi zilizopo na kupatiwa huduma hizo bure na kupata haki kwa wakati.
“Lengo hasa la huduma hii ni kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake katika mamlaka husika za utoaji haki na wakati”alisema Shaiba.
Alisema sambamba na huduma hiyo kupitia sekretarieti, wizara katika ofisi zake za makao makuu pia imepokea malalamiko ya wananchi yanayohusiana na haki na utoaji wa ushauri na maelekezo ya kufuatilia haki zao.
“Wizara imewafahamisha wananchi kuwa huduma za kisheria kwa watu wenye uhitaji ambao wanakosa huduma za aina hiyo wanaweza kupata huduma hiyo bila malipo ambapo utaratibu huo umefanyika wakati wizara ipo katika hatua ya mwisho ya kutunga sheria ya msaada” alisema.
Alisema mpango huo ulianzishwa mwaka 2012, ili kuwezesha asasi au mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kupanua wigo wa huduma ya msaada wa kisheria kwa wahitaji husuasan wananchi wanaoishi kwenye maeneo ambayo kwa namna moja au nyingine awawezi kupata wala kulipia gharama za mawakili nchini.
Wakili Mkuu wa Serikali Charles Mmbando, aliwaomba mawakili na tasisi zote zinazojishughulisha na hitohaji wa huduma za kisheria nchini kuendelea na utoaji wa huduma hiyo vizuri kwa wananchi wasio na uwezo wa kumudu kulipia gharama za mawakili.
“Nachukua nafasi hii kuwasihi wananchi wasio na uwezo hasa wa maeneo ya vijijini kwenda katika tasisi hizo na nyinginezo ambazo zinatoa  huduma za msaada wa kisheria kama huduma kwa jamii inayozizun guka” alisema Mmbando.


Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Charles Mmbando,akizungumza na waandishi wa habari,Dar es Salaam,jana kuhusu kutumia mpango wa huduma za msaada wa kisheria kupitia sekeretarieti ya msaada wa kisheria na mashirika kwa ajili hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini  kutoka  Wizara hiyo, Shaiba Bulu. Picha na Elisa Shunda




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni