Jumatatu, 9 Mei 2016

WANANCHI WAHAMASISHWA KUWEKEZA
























Kaimu Meneja Msaidizi wa Masoko ya Ndani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Genes Gos Kimaro,akifafanua jambo katika mkutano huo.

NA:ELISA SHUNDA,DAR


BENKI kuu ya Tanzania (BOT), imewahamasisha wanachi kutumia soko la dhamana la serikali kwa kuwekeza, na mali zao zitakuwa katika hali ya usalama.
Pia iewataka watu wa Afrika ya Mashariki kuja kuwekeza kupitia dhamana la soko hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko ya fedha, Alexander Ng’winamila, alisema katika uwekezaji huo tasisi nyingi zimeonekana zikitumia dhamana hizo lakini hali ya wananchi imeonekaana kuwa duni.
“Napenda kuwahamasisha wananchi kutumia soko la dhamana la serikali kuwekeza katika dhamana ya muda mfupi na muda mrefu kwani mali zao zitakuwa salama ” alisema Ng’winamila.
Alisema endapo mwananchi atajiunga na soko la dhamana la serikali ataweza kupatiwa mkopo kutokana na dhamana aliyoiweka na kurudisha kidogo kidogo huku akipata fidia.
“Dhamana ya serikali ya muda mfupi ni ukitaka kujiunga ni Sh. 500,000, na dhamana za muda mrefu ni Sh. milioni 1 hadi 50 na hivyo tunawaomba wananchi mjitokeze kuwekeza ili kuweza kujiongezea kipato na maendeleo”alisema.
Meneja Msaidizi masoko ya ndani Genes Kimaro, alisema wananchi anayetaka kujiunga wafike kwa mawakala wao waliopo nchi nzima ili kuweza kufungua account na kuingiziwa kumbukumbu ili kuweza kufikishwa  taarifa zao BOT, kwajili ya kusajiliwa.
Alisema baada ya kusajiliwa kila ijumaa wale wote waliofungua account watapatiwa matangazo ambayo kila jumatano wataweza kushiriki katika mnada wa serikali kupitia soko la dhamana alilojiunga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni