DAR ES SALAAM
meelezwa kuwa asimilia 65 ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani watu wenye albinism wamefanyiwa vitendo vya ukatili nchini Malawi mwaka 2015.Akizungumza na wanahabari jijini dare s salaam mkurugenzi mkuu wa shirika la under the same sun BW. PETER ASH amesema kuwa vitendo vya ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi bado vinaendelea hivyo kutoa rai kwa serikali kushirikiana na serikali ya Malawi kukabiliana na vitendo hivyo.
Aidha BW.ASH ameushukuru uongozi wa awamu ya tano kwa kumteuwa naibu waziri mwenye ulemavu wa ngozi akiamini kuwa naibu waziri huyo atasaidia kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi.
Mkurugenzi Mkuu wa Under the Same Sun Bw.Peter Ash
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Tanzania bi. VICKY NTETEMA ametoa wito kwa serikali kuharakisha kutolewa kwa hukumu kwa watu wote watakao bainika wakifanya vitendo vya ukatili.
Mkurugenzi Msaidizi Tanzania Under the Same Sun Bi.Vicky Ntetema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni